RAIS wa Shirikisho la Soka la Ulaya aliyefungiwa Michel Platini ametoka akiwa na furaha baada ya kusikilizwa kwa rufani yake na kamati ya rufani ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA na ana matumaini ya kusafisha jina lake kabla ya michuano ya Euro 2016. Platini na rais wa FIFA Sepp Blatter wote wamefungiwa miaka nane kujishushughulisha na masuala ya soka Desemba mwaka jana kufuatia uchunguzi wa kamati huru ya maadili ya shirikisho hilo kuhusiana na malipo ya paundi milioni 1.3 yaliyosainiwa na Blatter kwenda kwa Platini mwaka 2011. Tume ya uchunguzi ya kamati ya maadili inataka kuangalia uwezekano wa kuongeza adhabu hiyo hivyo kumaanisha Blatter na Platini ambao wote wamekanusha kufanya lolote baya wanaweza kufungiwa maisha. Platini alianza kusikiliza rufani yake jana akipinga adhabu hiyo huko Zurich na ameonyesha kufurahishwa na jinsi mambo yanavyokwenda. Blatter ambaye naye pia alikata rufani kupinga adhabu hiyo yeye yak wake inatarajiwa kusilikilizwa leo.
No comments:
Post a Comment