KLABU ya Manchester United imemtangaza kiungo wa zamani wa timu hiyo Nicky Butt kuwa mkuu wa akademi ya soka. Butt mwenye umri wa miaka 41, aliibuka akitokea vikosi vya chipukizi vya United na kufanikiwa kucheza mechi 387 kati ya mwaka 1992 mpaka 2004. Nguli huyo amekuwa akifanya kazi kama kocha wa kikosi cha akiba na kocha wa kikosi cha vijana wa chini ya umri wa miaka 19 toka amerejea katika klabu hiyo mwaka 2012. Makamu mwenyekiti wa United, Ed Woodward amesema Butt ana urithi na utamaduni wa klabu katika damu yake hivyo anadhani ni chaguo sahihi katika nafasi aliyopewa.
No comments:
Post a Comment