MWAMUZI wa soka amepigwa risasi na kufa nchini Argentina na mchezaji chipukizi kufuatia kumuonyesha kadi nyekundu. Tukio hilo limetokea katika mji wa Cordoba wakati mchezaji huyo alipomfyatulia risasi mwamuzi dakika chache baada ya kumtoa nje kwa nyekundu kwa kosa la kumpiga mchezaji mwenzake. Mchezaji mwingine Walter Zarate naye pia alipigwa risasi na kukimbizwa hospitali huku hali yake ikiripotiwa kuwa mbaya. Polisi wanasema mwamuzi huyo Cesar Flores mwenye umri wa miaka 48 aliuawa baada ya kupigwa risasi mara tatu, moja kichwani, shingoni na kifuani.
No comments:
Post a Comment