Monday, February 8, 2016

PIRLO AMMWAGIA SIFA OZIL.

KIUNGO mkongwe Andrea Pirlo amemtaja kiungo wa Arsenal Mesut Ozil kuwa mchezaji mbunifu zaidi barani Ulaya. Ozil ametoa pasi za mwisho 16 katika mashindano mpaka sasa msimu huu, huku akizidiwa pekee na nyota wa Borussia Dortmund Henrikh Mkhitaryan ambaye ametengenezea nafasi wenzake mara 17. Pirlo ambaye alijiunga na New York City FC baada ya kuondoka Juventus majira ya kiangazi mwaka jana, ameonyesha kumuhusudu nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani na hivi karibuni kumtaja kuwa miongoni mwa wachezaji wakali zaidi katika Ligi Kuu. Akihojiwa Pirlo amesema Ozil ndio mchezaji mbunifu zaidi Ulaya kwasasa kwani ametengeneza nafasi nyingi sana kwa washambuliaji ambao amecheza nao. Pirlo aliendelea kudai kuwa kwa jinsi Ozil alivyo na maoni ya mbali hadhani kama kuna mwingine zaidi yake kwasasa.

No comments:

Post a Comment