Monday, February 8, 2016

LEICESTER KUMUWANIA KIUNGO WA FEYENOORD MAJIRA YA KIANGAZI.

KLABU ya Leicester City inatajwa kupewa nafasi kubwa ya kumsajili kiungo wa klabu ya Feyenoord Tonny Vilhena majira ya kiangazi. Kiungo huyo anatarajiwa kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu hivyo kumaanisha kuwa atakuwa huru kwa ajili ya usajili huku Feyenoord wakidaiwa bado kuhitaji huduma ya nyota huyo. Lakini Leicester City ambao wanongoza Ligi Kuu kwa tofauti ya alama sita wanatajwa kuongoza mbio za kumuwani kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21. Jarida la The Hinckley Times limedai kuwa klabu hiyo imekuwa ikimfuatilia katika mechi kadhaa msimu huu na wana uhakika wa kuzipiku klabu za Swansea City, West Bromwich Albion na Sunderland ambazo zote zimeonyesha nia ya kumtaka.

No comments:

Post a Comment