KLABU ya Manchester United imetangaza kuwa Jukwaa la Upande wa Kusini katika uwanja wake wa Old Trafford litabadilishwa na kupewa jina la Sir Bobby Charlton. Charlton enzi zake aliichezea United mechi 750 na kufunga mabao 249 ambayo yaliisaidia timu hiyo kunyakuwa mataji matatu ya Ligi Kuu na moja la Ulaya mwaka 1968. Nguli huyo pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Uingereza kilichotwaa taji la Kombe la Dunia mwaka 1966 akifunga mabao matatu katika michuano hiyo.
Akizungumza na wanahabari kuhusiana na hilo Charlton amesema ni heshima kubwa nay eye pamoja na familia yake wanajivunia kwa klabu hiyo kuamua kuchagua jina lake kutumika katika upande mmoja wa uwanja. Charlton aliendelea kudai kuwa United imekuwa sehemu muhimu katika maisha yake na ana kumbukumbu nyingi nzuri ikiwemo mabao aliyofunga wakati akiwa mchezaji na hata nafasi yake ya ukurugenzi aliyonayo hivi sasa.
No comments:
Post a Comment