MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Brazil, Neymar amedai kuwa mbinu waliyotumia kupiga penati ya kipekee Lionel Messi na Luis Suarez katika ushindi wa mabao 6-1 waliopata Barcelona dhidi ya celta Vigo jana, ilitakiwa kumuhusisha yeye. Messi aliushangaza umati uliojitokeza Camp Nou wakati alipotoa pasi mpira wa penati kwenda kwa Suarez na kumfanya nyota huyo kuunga hat-trick katika mchezo huo. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina angeweza kufunga mwenyewe penati hiyo na kufikisha bao lake la 300 lakini aliamua kutofunga na kutoa pasi kwa Suarez jambo liliwashangaza na kuwavutia mashabiki wengi wa soka duniani kote. Akihojiwa Neymar amesema wamesema wamekuwa wakifanya mazoezi ya kupiga penati ya aina hiyo lakini kwa ajili yake. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa jana ilishindikana kwasababu Suarez ndio alikuwa karibu zaidi na mpira hivyo akafunga jambo ambalo ni zuri kwani wamepata ushindi waliohitaji.
No comments:
Post a Comment