NAHODHA wa Manchester City, Vincent Kompany amesema itakuwa ni ujinga wakisahau historia yao na kutopigania taji. City walichapwa mabao 2-1 nyumbani na mahasimu wao Tottenham Hotspurs na kuwafanya kubaki katika nafasi ya nne katika msimamo wakipishana alama sita na vinara Leicester City. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Kompany amesema haitawezekana kwa namna yeyote kukata tama ya kupigania taji na wanachofanya hivi sasa ni kuimarika. City sasa wanakuwa wamepoteza mechi mbili kati ya tatu zilizopita za Ligi Kuu moja ikiwa dhidi ya Leicester, toka itangazwe kuwa meneja wa klabu hiyo Manuel pellegrini ataondoka kiangazi na nafasi yake kuchukuliwa na Pep Guardiola. Kompany anaamini wangeweza kucheza vyema zaidi ya jana lakini ana imani wataimarika na kuendelea na mapambano.
No comments:
Post a Comment