BEKI wa kimataifa wa Ufaransa, Mathieu Debuchy amekiri kukerwa na Arsene Wenger baada ya meneja huyo wa Arsenal kuzuia uhamisho wake wa mkopo kwenda Manchester United. Debuchy amejiunga kwa mkopo Bordeaux mpaka mwishoni mwa msimu huu kufuatia kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza msimu huu. Toka arejee kutoka katika majeruhi Debuchy amekuwa chaguo la pili katika kikosi cha Wenger ambapo nafasi hiyo amekuwa akipewa Hector Bellerin. Beki huyo wa zamani wa Newcastle United aliamua kwenda Ufaransa baada ya kunyimwa nafasi ya kujinga na United kwa mkopo. Debuchy alikaririwa na mtandao wa Canal akidai kuwa United waliwasiliana na wawakilishi wake wakati dirisha la usajili likielekea mwishoni lakini suala hilo lilishindikana baada ya Wenger kumuhabalisha kuwa hawezi kusaidia wapinzani wake.
No comments:
Post a Comment