NYOTA wa Paris Saint-Germain-PSG, Marco Verratti ameongeza mkataba wa mwaka mmoja ambao utamuweka katika klabu hiyo mpaka mwaka 2020. Verratti mwenye umri wa miaka 23 alijiunga na PSG Julai mwaka 2012 na tayari ameshaichezea mechi 155 huku wakishinda mataji matatu mfululizo ya Ligue 1. Akihojiwa nyota huyo wa kimataifa wa Italia amesema amefurahi kuongeza mkataba kwani hiyo inaonyesha jinsi gani klabu hiyo ilivyokuw ana imani naye. Verratti amesema anaipenda PSG na analipenda jiji la Paris hivyo ataendelea kujitoa kwa kila hali kuhakikisha wanashinda mataji na kuwa klabu bora Ulaya.
No comments:
Post a Comment