KLABU za Stoke City na Everton ndio zilizokamilisha usajili uliotumia fedha nyingi kabla ya dirisha dogo la usajili la Januari halijafungwa jana usiku na kufanya matumizi kufikia paundi milioni 175. Klabu za Ligi Kuu sasa zinakuwa zimetumia bilioni 1.04 katika usajili kwa msimu huu wa 2015-2016 ikiwa ni kiwango cha juu zaidi kulinganisha na mwaka jana. Stoke walivunja rekodi yao kwa kumsajili Giannelli Imbula kutoka Porto kwa kitita cha paundi milioni 18.3 huku Everton wao wakitumia kitita cha paundi milioni 13.5 kumnasa mshambuliaji wa Lokomotiv Moscow Oumar Niasse. Rekodi iliyowekwa katika usajili wa msimu uliopita ilikuwa ni paundi milioni 965. Hata hivyo, habari kubwa iliyotamba jana katika vyombo mbalimbali vya habari kuelekea kufungwa kwa dirisha la usajili ni taarifa za Manchester City kutangaza kuwa meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola ndio atakayechukua nafasi ya Manuel Pellegrini mwishoni mwa msimu huu.
Tuesday, February 2, 2016
STOKE, EVERTON ZAFUNGA USAJILI KWA KISHINDO.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment