Tuesday, February 2, 2016

MANCINI ALIMWA ADHABU KWA MATUSI.

MENEJA wa Inter Milan, Roberto Mancini amelimwa adhabu ya mechi moja baada ya kuonyesha ishara ya kudhalilisha wakati wa mchezo wa Serie A waliofungwa na mahasimu wao AC Milan. Meneja huyo wa zamani wa Manchester City alitolewa katika benchi lake la ufundi kufuatia tukio hilo wakati Inter walippata kichapo kizito cha mabao 3-0 kutoka kwa Milan Jumapili iliyopita. Mancini alifanya tukio hilo kufuatia kukasirishwa kwa timu yake kunyimwa penati baada ya golikipa wa Mila Gianluigi Donnarumma kuchezea faulo mshambuliaji wa Inter, Eder. Mbali na adhabu hiyo ya kufungiwa, Mancini mwenye umri wa miaka 51 pia amelimwa faini ya euro 5,000.

No comments:

Post a Comment