USAJILI wa China umevunja rekodi kwa mara ya tatu ndani ya siku 10 baada ya klabu ya Jiangsun Suning kutumia kitita cha paundi milioni 38.4 kwa ajili ya kumsajili Alex Teixeira kutoka Shakhtar Donetsk. Kiungo huyo wa Brazil aliyekuwa akiwindwa na Liverpool, amekuwa mchezaji mwingine nyota kuhamia katika Ligi Kuu ya China. Kiungo wa zamani wa Chelsea Ramires naye alisajiliwa na Jiangsun Suning kwa kitita cha paundi milioni 25. Hatua hiyo inafuatia baada ya Guangzhou Evergrande Taobao kumsajili Jackson Martinez kwa kitita cha paundi milioni 31 kutoka Atletico Madrid. Jumla ya kiasi kilichotumika kwa wachezaji hao watatu ni paundi milioni 94.
No comments:
Post a Comment