KLABU ya Manchester City imepata ahueni kufuatia taarifa kuwa nahodha wake Vincent Kompany ameanza mazoezi katika kikosi cha kwanza. Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alikuwa nje ya kikosi cha City toka alipotolewa katika mchezo dhidi ya Sunderland Desemba mwaka jana kutokana na majeruhi ya ugoko. City imefanikiwa kutofungwa katika mechi sita za ligi walizocheza toka beki huyo mwenye umri wa miaka 29 alipoumia lakini kati ya hizo wametoa sare mechi tatu. Meneja wa City Manuel Pellegrini alibainisha beki huyo kwasasa anaendelea vyema na anaweza kumtumia katika mchezo wa kesho dhidi ya Leicester City.
No comments:
Post a Comment