MAKUNDI ya mashabiki wa Liverpool wamepanga kutoka nje ya uwanja kupinga bei kubwa za kiingilio wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Sunderland kesho utakaochezwa katika Uwanja wa Anfield. Makundi hayo ya The Spion Kop 1906 likisaidiwa Spirit of Shankly, wamewataka mashabiki kuondoka uwanjani katika dakika ya 77 kupiga bei ya paundi 77 kwa tiketi za jukwaa kuu jipya. Klabu hiyo imetangaza ongezeko hilo la bei kwa mwezi ujao kutoka paundi 59 iliyokuwepo kabla. Vikundi hivyo vinadai kuchukizwa na hatua hiyo kwasababu hakuna sababu yeyote iliyotolewa na wamiliki kuhusiana na beki hizo kupanda.
No comments:
Post a Comment