Friday, February 5, 2016

AGUERO MCHEZAJI BORA WA JANUARI.

MSHAMBULIAJI nyota wa Manchester City, Sergio Aguero ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Januari wa Ligi Kuu. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27, amefunga mabao matano katika mechi nne alizocheza na kumfanya kuikwaa tuzo hiyo kwa mara ya kwanza msimu huu. Kikosi cha City kinachonolewa na Manuel Pellegrini hakijafungwa mwezi uliopita huku Aguero akifunga mabao mawili katika sare ya mabao 2-2 waliyopata dhidi ya West Ham United na mengine mawili katika mchezo walioshinda mabao 3-0 dhidi ya Crystal Palace. Aguero amewapiku Dele Alli wa Tottenham Hotspurs, Virgin van Dijk wa Southampton, Roberto Firmino wa Liverpool, Jermain Defoe wa Sundeland na Kasper Schmeichel wa Leicester City ambao nao walikuwepo katika king’anyiro hicho. Kocha wa Southampton, Ronald Koeman ndiye aliyenyakuwa tuzo ya kocha bora wa mwezi baada ya kushinda mechi tatu kati ya nne walizocheza Januari.

No comments:

Post a Comment