Friday, February 12, 2016

TETESI MBALIMBALI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.

JOSE Mourinho anadaiwa kuwa atawasajili Neymar, Gareth Bale na Raphael Varane Old Trafford wakati atakapokabidhiwa mikoba ya kuinoa Manchester United.
Chanzo: Fichajes.net

PEP Guardiola anadaiwa kutaka kumleta golikipa wa Inter Milan Samir Handanovic Manchester City msimu ujao kufuatia kuwepo wasiwasi wa kuondoka kwa Joe Hart.
Chanzo: Corriere dello Sport

KLABU ya Arsenal, inajiandaa kutenga ofa ya paundi milioni nane kwa ajili ya kiungo wa West Ham United Reece Oxford huku Arsene Wenger akipania kuzizidi maarifa Manchester United na Manchester City ambao nao wanamuwania.
Chanzo: Daily Mirror

BEKI wa Real Madrid Alvaro Arbeloa amekataa ofa ya paundi milioni nane kwenda kujiunga na klabu ya Shanghai Shengua ya China pamoja na mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool kukaribia kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu.
Chanzo: Marca

BAADA ya uhamisho wa Merino mwenye umri wa miaka 19 kuvunjika katika kipindi cha dirisha dogo Januari mwaka huu, Osasuna na Borussia Dortmund sasa wamefikia makubaliano na kiungo huyo chipukizi sasa anatarajiwa kujiunga na BVB majira ya kiangazi.
Chanzo: Kicker

KLABU ya Arsenal inatarajiwa kuvaana na AC Milan uso kwa uso katika kinyang’anyiro cha kumuwania kiungo wa Nice Vincent Koziello mwenye umri wa miaka 20.
Chanzo: Express

KLABU ya Paris Saint-Germain-PSG inadaiwa kuwa tayari kumpa ofa nyota wa Barcelona Neymar mshahara wa euro milioni 40 kwa mwaka.
Chanzo: UOL

KLABU ya Manchester United inadaiwa kutaka kumuwania mshambuliaji wa Inter Milan Mauro Icard.
Chanzo: Tuttosport

No comments:

Post a Comment