Friday, February 12, 2016

ROBINHO AREJEA TENA BRAZIL.

KLABU ya Atletico Mineiro ya Brazil imethibitisha kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester City na Real Madrid, Robinho. Katika taarifa yake klabu hiyo yenye maskani yake huko Belo Horizonte imedai kuwa wamemsajili Robinho kwa mkataba wa miaka miwili. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 32 ambaye pia amewahi kucheza AC Milan, alikuwa mchezaji huru toka kuanza kwa mwezi huu baada ya kumaliza mkataba wake wa miezi sita na klabu ya Guangzhou Evergrande wa China. Robinho alifanikiwa kufunga mabao matatu katika kipindi aliwatumikia mabingwa hao wa Ligi Kuu ya China na Mineiro sasa wamefanikiwa kumnasa na kuwazidi maarifa wenzao Santos ambao nao walimhitaji.

No comments:

Post a Comment