Friday, February 12, 2016

ARSENAL KUCHEZA NA NYOTA WA MLS KIANGAZI.

KLABU ya Arsenal inatarajiwa kucheza na wachezaji nyota wa Ligi Kuu ya marekani-MLS wakati wa kipindi cha maandalizi ya msimu ujao Julai 28 huko Calfornia. Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa kabla ya ratiba ya mchezo dhidi ya Chivas ya Mexico utakaofanyika jijini Los Angeles Julai 31 mwaka huu. Manchester United, Everton, Chelsea na Tottenham Hotspurs ni miongoni mwa klabu zingine za Uingereza zilizowahi kucheza na nyota hao wa Marekani. Kamishna wa MLS, Don Garber amesema wanayo furaha kubwa kuikaribisha Arsenal moja ya klabu kubwa duniani ili kuja kushindana dhidi ya wachezaji bora wa MLS.

No comments:

Post a Comment