Friday, February 19, 2016

TP MAZEMBE KUWANIA TAJI LA TATU LA SUPER CUP BILA SAMATTA.

MABINGWA wa soka wa Afrika, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-DRC kesho wanatarajiwa kujitupa uwanjani kuvaana na Etoile du Sahel ya Tunisia katika mchezo wa Super Cup. Mchezo huo ambao hutumika kama kiashiria cha kuanaza msimu mpya wa michuano ya vilabu barani Afrika hukutanisha bingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambaye ni Mazembe na bingwa wa Kombe la Shirikisho ambao ni Etoile. Katika mchezo huo utakaofanyika jijini Lubumbashi, Mazembe watakuwa wakifukuzia taji lao la tatu la Super Cup baada ya kunyakuwa mwaka 2010 na 2011. Mazembe watakuwa bila mshambuliaji wake nyota wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta ambaye amajiunga na klabu ya Genk ya Ubelgiji katika usajili wa dirisha dogo Januari. Mabao aliyofunga Samatta yaliisaidia sana Mazembe kutwaa ubingwa huo huku mwenyewe akiteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani.

No comments:

Post a Comment