Friday, February 19, 2016

POGBA AIFUNGULIA MILANGO MAN CITY.

KIUNGO wa Juventus, Paul Pogba amefungua milango ya kujiunga na Manchester City baada ya kudai nafasi ya kufanya kazi na Pep Guardiola inaweza kumfanya aimarike zaidi. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwaniwa na klabu kadhaa barani Ulaya katika kipindi cha miaka miwili iliyopita huku Barcelona wakidaiwa ndio wenye nafasi kubwa ya kumnasa kiungo huyo wa zamani wa Manchester United. Lakini kwa jinsi Pogba alivyozungumzia kuhusudu uwezo wa Guardiola ambaye msimu ujao atatua Etihad kunabadili kabisa uelekeo atakaochukua majira ya kiangazi. Akihojiwa Pogba amesema Guardiola ana uzoefu mkubwa na aina ya ocha ambaye huwa anakuwa na ushawishi mkubwa kwa wachezaji wote. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa amekuwa akimhusudu kocha huyo na ana matumaini siku moja atakuja kufanya naye kazi.

No comments:

Post a Comment