MENEJA wa Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino amesema Dele Alli bado ana vitu vingi vya kujifunza baada ya chipukizi huyo wa kimataifa wa Uingereza kuonekana akimkwatua mchezaji mwenzake kwa makusudi katika sare ya bao 1-1 waliyopata dhidi ya Fiorentina katika mchezo wa Europa League uliochezwa jana. Alli mwenye umri wa miaka 19, alilimwa kadi kwa kumchezea vibaya Nenad Tomovic na kunaswa akimkanyaga tena beki huyo wakati akiwa chini. Pochettino amesema hakuliona tukio hilo kwa muda ule lakini amepanga kuzungumza na kiungo huyo baada ya kuona marudio ya picha za video. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa wanatakiwa kujaribu kumfundisha kwani bado mdogo na kuna vitu vingi anapswa kujifunza kuhusu soka.
No comments:
Post a Comment