Tuesday, March 8, 2016

ARSENAL YATINGA ROBO FAINALI FA.



KLABU ya Arsenal imekumbwa na balaa la majeruhi pamoja na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la FA jana. Katika mchezo huo Arsenal ilifanikiwa kuitwanga Hull City mabao 4-0 mabao ambayo yalifungwa na Olivier Giroud dakika ya 41 na 71 na Theo Walcott dakika ya 77 na 88 na kuifanya timu hiyo kuendeleza rekodi yake ya kutofungwa kwa miaka mitatu katika michuano hiyo. Hata hivyo, ushindi huo haukuja kwa rahisi kwani Arsenal ililazimika kuwatoa wachezaji wake watatu akiwemo Aaron Ramsey, Per Mertesacker na Gabriel Paulista ambao waliumia. Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema ameshtushwa na majeruhi hayo lakini ana matumaini hayatakuwa ya muda mrefu.



Arsenal inatarajiwa kukwaana na Watford Jumapili katika mchezo wa robo fainali ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment