Tuesday, March 8, 2016

CHAMPIONS LEAGUE: RONALDO ATUPIA BAO LA 40 WAKATI MADRID IKITINGA ROBO FAINALI KWA KISHINDO.



MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefunga bao lake la 40 msimu huu wakati timu hiyo ikitinga robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuichapa Roma kwa jumla ya mabao 4-0. Katika mchezo huo wa jana Ronaldo alifunga bao la kuongoza dakika 64 kabla ya kutengeneza lingine lililofungwa na James Rodriguez katika dakika 68 na kuwafanya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 kama waliopata katika mchezo wao wa mkondo wa kwanza. Madrid wanaonolewa na Zidane kwasasa wako nyuma ya vinara wa La Liga Barcelona kwa alama 12 huku wakiwa wameondolewa katika michuano ya Kombe la Mfalme hivyo kufanya Ligi ya Mabingwa Ulaya kuwa michuano pekee ambayo inaweza kuwapa taji msimu huu. Katika mchezo mwingine uliochezwa jana Wolfsburg ya Ujerumani nao walifanikiwa kutinga robo fainali kwa mara ya kwanza baada ya kuichapa Genk kwa bao 1-0 na kuwafanya kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-2.

No comments:

Post a Comment