MENEJA wa Manchester United, Louis van Gaal amesema lazima washinde kila mechi katika michezo tisa ya Ligi Kuu waliyobaki nayo baada kipigo walichopata kutoka kwa West Bromwich Albion jana. Van Gaal amesema nafasi tatu za juu ndio lengo la United wakati akifanya mahojiano kabla ya mchezo lakini kipigo cha bao 1-0 waichopata kimewafanya wabakie katika nafasi ya sita wakiwa alama tano nyuma ya Arsenal walioko nafasi ya tatu na nne dhidi ya Manchester City ambao pia wana mchezo mmoja mkononi. Kwa upande mwingine West Ham United wako katika nafasi ya tano wakitofautiana alama mbili na United baada ya kushinda mchezo woa dhidi ya Everton kwa mabao 3-2. Mechi walizobakiwa nazo United ni dhidi ya Manchester City, Tottenham Hotspurs, Leicester City, Crystal Palace, Everton, Aston Villa, West Ham United, Norwich City na Bournemouth. Van Gaal amesema kwa nafasi waliyopo wanahitaji alama 27 na ili hilo liewezekane inabidi washinde mechi zote tisa zilizobakia.
No comments:
Post a Comment