Monday, March 7, 2016

TERRY KUIKOSA PSG.

MENEJA wa Chelsea, Guus Hiddink amethibitisha kuwepo uwezekano mkubwa wa John Terry kutokuwa fiti kwa ajili ya mchezo wao wa hatua ya 16 bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain-PSG. Terry mwenye umri wa miaka 35 ameshakosa mechi tano za mashindano yote kwa klabu hiyo toka alipopata majeruhi ya msuli wa paja katika mchezo walioshinda mabao 5-1 dhidi ya Newcastle United. Ijumaa iliyopita Hiddink alikuwa na matumaini ya beki huyo mkongwe kupona kwa wakati kwa ajili ya mchezo huo lkini sasa hali imebadilika kutokana na majeraha yake kupona taratibu. Hiddink amesema kutokana na hali ilivyo hakuna uwezekano wa Terry kuwepo katika mchezo wao huo wa Jumatano.

No comments:

Post a Comment