Monday, March 7, 2016

FIRMINO AITWA BRAZIL KUCHUKUA NAFASI YA KAKA.

MSHAMBULIAJI wa Liverpool Roberto Firmino ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kwa ajili ya mechi zijazo za kufuzu Kombe la Dunia akichukua nafasi ya Kaka aliyeumia. Kaka alipata mazoezi ya msuli wakati wakiwa mazoezini Jumamosi iliyopita na kumfanya kukosa mchezo ambao Orlando City walitoka sare mabao 2-2 dhidi ya Real Sale Lake katika mchezo wao wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Marekani-MLS. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 33 anarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda na hivyo kupelekea kuondolewa katika kikosi cha Brazil ambacho kitachuana na Uruguay na Paraguay baadae mwezi huu. Firmino ambaye amekuwa katika kiwnago kizuri katika msimu huu aliongezwa katika kikosi hicho jana.

No comments:

Post a Comment