MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Diego Costa amekanusha kumng’ata Gareth Barry wakati wa mchezo wao wa robo fainali wa Kombe la FA ambao walifungwa mabao 2-0 na Everton. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania alitolewa kufuatia kuvaana na kiungo huyo wa Everton dakika ya 84 ya mchezo huo uliofanyika Goodison Park. Msemaji wa Chelsea amesema Costa alizungumza na maofisa wa klabu hiyo na kueleza kujutia tukio alilomfanyia Barry ambalo lilipelekea kulimwa kadi nyekundu lakini pia ameweka wazi kuwa hakung’ata mchezaji huyo kama inavyodhaniwa na wengi. Meneja wa Chelsea, Guus Hiddink amedai Everton walimkorofisha kwa makusudi Costa ambaye alikuwa akichuana vikali na Barry muda wote wa mchezo.

No comments:
Post a Comment