Friday, March 11, 2016

NEWCASTLE YAMTIMUA MCCLAREN, BENITEZ ANUKIA.

KLABU ya Newcastle United hatimaye imeamua kumtimua meneja wake Steve McClaren kutokana na matokeo mabovu ambaye yameendelea kuiandama timu hiyo. Meneja huyo wa zamani wa timu ya taifaya Uingereza amefanikiwa kushinda mechi sita kati ya 28 za Ligi Kuu toka achukue mikoba ya kuinoa Newcastle ambao wanashikilia nafasi ya 19 katika msimamo wa ligi kwasasa. McClaren na kikosi chake walizomewa na mashabiki kufuatia kipigo cha mabao 3-1 walichopata Jumamosi iliyopita kutoka kwa Bournemouth kwenye Uwanja wa St James Park, kikiwa ni kipigo chao cha tatu mfululizo. Meneja wa zamani wa Liverpool, Chelsea, Real Madrid na Inter Milan, Rafa Benitez ndio inadokezwa atachukua nafasi ya McClaren. McClaren alisaini mkataba wa miaka mitatu Juni mwaka jana baada ya Newcastle kuepuka balaa la kushuka daraja mwishoni mwa msimu uliopita.


No comments:

Post a Comment