KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque anafahamu mtu ambaye atachukua nafasi yake katika kikosi cha nchi hiyo baada ya michuano ya Euro 2016. Del Bosque mwenye umri wa miaka 65, tayari ameshatangaza nia yake ya kujiuzulu baada ya kumalizika kwa michuano hiyo itakayorindika huko Ufaransa Juni na Julai. Del Bosque amesema una uhakika wa nani anayemtaka kcuhukua nafasi yake pindi atakapoondoka lakini hawezi kumsema kwasasa. Akizungumza na gazeti la Punto Pelota kuhusiana na suala hilo, Del Bosque alikataa kutaja jina la mbadala wake lakini akadi tayari anamfahamu.
No comments:
Post a Comment