Tuesday, March 1, 2016

PIQUE ADAI HAWEZI KUJIUNGA NA MAN CITY KUTOKANA NA MAPENZI ALIYONAYO KWA MAN UNITED.

BEKI wa Barcelona, Gerrard Pique amesema anaipenda sana Manchester United kiasi ambacho hataweza kwenda kusajiliwa Manchester City pamoja na Pep Guardiola kukubali kuchukua mikoba ya kuinoa timu hiyo. Guardiola alimfanya Pique mwenye umri wa miaka 29 kuwa usajili wake namba moja baada ya kuchukua mikoba ya kuinoa Barcelona mwaka 2008 na beki huyo kuja kung’aa na kuwa mmoja kati ya mabeki bora kabisa duniani. Pique ambaye alikwenda Old Trafford mwaka 2004, alishindwa kabisa kujiimarisha katika kikosi cha kwanza cha United kilichokuwa chini ya Sir Alex Ferguson lakini ameeleza kuwa na mapenzi na klabu hiyo. Nyota huyo amesema kwasasa ana furahia kuwepo Barcelona na anategemea kuwepo hapo kwa kipindi kirefu kijacho ila klabu yake ya pili anayoipenda ni United. Pique aliendelea kudai kuwa kwa jinsi anavyoipenda United hadhani kama anaweza kwenda kusajiliwa na mahasimu wao City pamoja na kwamba Guardiola ni kocha mkubwa.

No comments:

Post a Comment