MENEJA wa Leicester City, Claudio Ranieri amedai kuwa Tottenham Hotspurs ndio wanaopigiwa chapuo kunyakuwa taji la Ligi Kuu msimu huu. Spurs ambao wana alama mbili nyuma ya vinara Leicester huku kukiwa kumebaki mechi 11, hawajawahi kuongoza msimamo wa ligi toka wiki ya kwanza ya msimu wa 2009-2010. Lakini Ranieri ambaye kikosi chake kinakwaana na West Bromwich Albion baadae leo anaamini Spurs wanaweza kumaliza ukame wa miaka 55 na kutwaa taji hilo msimu huu. Meneja huyo raia wa Italia amesema Spurs wako imara kwa kila kitu ingawa watu hawaizungumzii sana na kwa maoni anadhani ndio wenye nafasi kubwa ya kutwaa taji. Spurs wanaweza kuleleni mwa msimamo wa ligi kama Leicester watafungwa katika mchezo wa leo huku na wao kushinda mchezo dhidi ya West Ham United kesho.
No comments:
Post a Comment