MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao amebainisha kuwa alikataa ofa kutoka klabu za China katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo ili aweze kuendelea kubakia Chelsea. Falcao aliyecheza kwa mkopo pia katika klabu ya Manchester United, amekuwa akipambana kupata muda wa kucheza toka atue Stamford Bridge na kutokuwa kwake fiti kumemfanya aanze katika mechi moja pekee ya Ligi Kuu msimu huu. Kulikuwa na tetesi kadhaa Januari zinazomuhusisha na kuondoka Chelsea na sasa amebainisha kuwa alikuwa na nafasi ya kufuata nyayo za Jackson Martinez, Ramires na Alex Teixeira kwa kwenda nchini China. Akihojiwa Falcao amesema ni kweli alishapata ofa mbili za klabu za China lakini alibakia Uingereza ili kujipa mwenyewe nafasi nyingine.

No comments:
Post a Comment