Monday, March 14, 2016

IBRAHIMOVIC ATANGAZA KUONDOKA PSG KIANGAZI.



MSHAMBULIAJI nyota wa Paris Saint-Germain-PSG Zlatan Ibrahimovic amesema anaweza kuondoka katika klabu hiyo majira ya kiangazi baada ya kuisaidia kunyakuwa taji la nne mfululizo la Ligi Kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1. Nyota huyo wa kimataifa wa Sweden alifunga mabao manne katika ushindi mnono wa mabao 9-0 waliopata dhidi ya Troyes na kutwaa taji hilo huku wakiwa wamebakiwa na mechi nane. Akihojiwa Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 34 amesema kwasasa anachofahamu yeye hatakuwepo PSG msimu ujao na amebakisha mwezi mmoja nusu pekee. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa kama wataweza kuubadili mnara maarufu uliopo jijini Paris wa Eiffel na kuweka sanamu lake basi anaweza kubakia PSG jambo ambalo hadhani kama linawezekana.

No comments:

Post a Comment