Friday, March 11, 2016

NGULI WA ARGENTINA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKA KWENYE NGAZI.

BEKI nguli wa zamani wa Argentina, Roberto Perfumo amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73 baada ya kuanguka mapema jana asubuhi. Perfumo ambaye kuzichezea klabu za Racing, River Plate na Cruzeiro ya Brazil enzi zake, alikimbizwa hospitalia baada ya kuanguka katika ngazi katika mgahawa mmoja huko Buenos Aires. Alifikizwa hospitalini akiwa katika hali mbaya kutokana na majeraha ya kichwa aliyopata kutokana na kuanguka na kufariki dunia baadae siku hiyo. Nguli wa soka wan chi hiyo Diego Maradona alituma salamu zake za rambirambi wa mchezaji mwenzake huyo wa zamani akiandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook kuwa haamini kama Perfumo hawako naye tena. Klabu zake za zamani nazo pia zimetuma salamu zao za rambirambi sambamba na wafanyakazi wenzake wa Ole na Futbol para Tudos ambako alikuwa akifanya kazi kama mwandishi na mtangazaji.

No comments:

Post a Comment