Friday, March 11, 2016

VAN GAAL AKIRI KUZIDIWA NA LIVERPOOL.

MENEJA wa Manchester United, Louis van Gaal amekiri kuwa kikosi chake kilizidiwa kila idara na Liverpool baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza michuano ya Europa League uliofanyika Anfield jana. Katika mchezo huo mabao Liverpool yaliwekwa kimiani na Daniel Sturridge kwa paneti na Roberto Firmino na ingeweza kuwa dhahama zaidi kama sio umahiri wa golikipa wa United David de Gea. Wachezaji wa zamani wa United Paul Scholes na Rio Ferdinand waliokuwa wachambuzi wa mchezo huo walikosoa vikali jinsi kikosi cha United kilivyocheza wakidai walikuwa wakicheza hovyohovyo bila mpangilio. Akihojiwa Van Gaal alikiri kikosi chake kushindwa kukabiliano na kasi kubwa ya Liverpool katika mchezo huo jambo ambalo hata yeye limemshangaza. Van Gaal amesema Liverpool walikuja na kasi kama hiyo walipocheza nao Old Trafford mwaka huu na wlaifanikiwa kuwafunga mabao 3-1, hivyo anashangaa ni kwanini wachezaji wake walishindwa kukabiliana na kasi hiyo jana.

No comments:

Post a Comment