SHIRIKISHO la Soka la Ulaya-UEFA, imefungua kesi ya kinidhamu dhidi ya Manchester United na Liverpool kufuatia vurugu zilizotokea jana katika mchezo wa marudiano wa Europa League uliofanyika katika Uwanja wa Old Trafford ambapo watu watano walikamatwa. Taarifa zinadai kuwa watu wanne waliokamatwa ni mashabiki wa Liverpool na mmoja wa United baada ya vurugu hizo kutokea katika Jukwaa la Mashariki. Tukio limetokea wakati United wakipoteza kwa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya mahasimu wao Liverpool baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo huo wa maruadiano. Polisi katika jiji la Manchester wamesema pamoja na kukamata mashabiki hao lakini kwa ujumla mashabiki wengi walikuwa watulivu na kuwashukuru kwa ushirkiano waliotoa.
No comments:
Post a Comment