Friday, March 18, 2016

ALABA AONGEZEWA SHAVU BAYERN.

BEKI wa Bayern Munich, David Alaba amesaini mkataba wa miaka mitatu na mabingwa hao wa Bundesliga. Alaba mwenye umri wa miaka 23 amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Pep Guardiola na mkataba huo mpya utamuweka Bayern mpaka 2021. Nyota huyo wa kimataifa wa Austria ametokana na matunda ya akademi ya Bayern na alipata nafasi ya kucheza mechi yake ya kwanza katika timu ya wakubwa mwaka 2010 huku akitumia nusu msimu kwa mkopo katika timu ya Hoffenheim. Alaba anacheza nafasi zote mbili kama kiungo wa kati na kiungo wa kukaba katika klabu hiyo toka alipobadili nafasi yake ya awali ya beki wa kati.

No comments:

Post a Comment