KIUNGO wa Manchester City, Yaya Toure ametajwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast kwa ajili ya mchezo ujao wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Sudan. Toure mwenye umri wa miaka 32, hajaitwa katika kikosi cha nchi hiyo toka alipoisaidia kutwaa taji la michuano hiyo Februari mwaka jana. Lakini kiungo huyo wa zamani wa Barcelona, ambaye amelitumikia taifa lake mara 100, anatarajiwa kurejea tena kwa ajili ya mchezo huo. Kocha wa Ivory Coast, Michel Dussuyer amesema Toure aliomba kupumzika jambo ambalo alieleweka ndio maana wakaamua kumuacha kwa muda. Dussuyer amesema amemuita tena kwakuwa anadhani sasa atakuwa tayari kwa ajili ya kuweza kuisaidia timu hiyo kufuzu na hata kutetea taji lao tena huko Gabon mwakani.
No comments:
Post a Comment