KLABU ya Inter Milan imethibitisha kumpa mkataba mpya wa miaka mitatu beki Yuto Nagamoto. Nyota huyo wa kimataifa wa Japan, ambaye amecheza mechi zaidi ya 170 akiwa na Inter amekubali mkataba huo mpya ambao utamuweka San Siro mpaka Juni 30 mwaka 2019. Msimu huu Nagamoto ameichezea Inter mechi 21 katika mashindano yote. Nagamoto mwenye umri wa miaka 29, ambaye alijiunga na Inter akitokea Tokyo FC mwaka 2011, amedai kuwa kukataa nafasi ya kujiunga na Manchester United Januari mwaka huu.
No comments:
Post a Comment