MENEJA wa West Bromwich Albion, Tony Pulis amedai kutokuwa na haraka ya kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. Pulis amebakisha mwaka mmoja mkataba wake wa sasa kumalizika na amesema atazungumza na mwenyekiti Jeremy Peace kuhusiana na mustabali wake ifikapo majira ya kiangazi. West Brom wako nafasi ya 11 katika msimamo wa Ligi Kuu, alama 13 juu ya eneo hatari huku wakiwa wamebaki na mechi saba kabla ya safari yao kuifuata Manchester City kesho. Akihojiwa Pulis mwenye umri wa miaka 58 amesema hana haraka kwasasa ya kusaini mkataba mpya hivyo anasubiri pindi msimu utakapomalizika ndio atakaa kuzungumzia suala hilo.
No comments:
Post a Comment