NAHODHA wa zamani wa Tottenham Hotspurs, Ledley King anaamini kocha Mauricio Pochettino anapswa kukataa ofa ya kwenda kujiunga na Manchester United. Spurs wako katika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu wakielekea mchezo wao wa Jumapili ambao watakuwa wenyeji wa United. Pochettino amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwaniwa na United kufuatia mustakabali wa Louis van Gaal kutoeleweka Old Trafford. Lakini King anadhani Pochettino anapswa kuendelea kuinoa Spurs ili kumalizia mipango aliyoweka wakati wakifukuzia taji la ligi huku kukiwa kumebaki michezo saba. King amesema wote wanafahamu United ni klabu kubwa lakini hadhani kama itakuwa sahihi kwa Pochettino kwenda huko hivi sasa.
No comments:
Post a Comment