MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amekiri atashindwa kuzuia hisia zake wakati kikosi chake kitakapovaana na Borussia Dortmund katika mchezo wa robo fainali ya Europa League kesho. Klopp ambaye aliinoa Dortmund kwa miaka saba kabla ya kuhamia Liverpool anatarajiwa kupokewa vyema katika Uwanja wa Signal Iduna Park. Meneja huyo mwenye umri wa miaka 48 aliiongoza Dortmund kushinda taji la Bundesliga mwaka 2011 na Kombe la DFB mara mbili huku akiifikisha klabu hiyo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2013 kabla ya kuondoka msimu uliopita. Akihojiwa Klopp amekiri kuingia katika uwanja wa Dortmund kwa mara nyingine akiwa kocha wa timu pinzani itakuwa ni changamoto kwake kwani bado anawafamu watu klabuni hapo. Meneja huyo alionngeza kuwa kutembea katika korido itakuwa kama kurejea nyumbani na hajahitaji mtu wa kumsaidia kwani anafahamu kila upande wa jukwaa na mahusiano yaliyopo.
No comments:
Post a Comment