Friday, April 1, 2016

PIRLO AMPIGIA DEBE POGBA.

KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Italia na Juventus, Andrea Pirlo amedai kuwa Paul Pogba atahitaji ada itakayovunja rekodi ya dunia kama akiamua kuondoka kwa mabingwa hao wa Serie A. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23, anawindwa na vilabu mbalimbali kutokana na kiwango bora alichoonyesha msimu huu. Pogba amekuwa akihusishwa na tetesi za kutakiwa na vilabu kadhaa lakini wakala wake Mino Raiola amesema mteja wake yuko tayari kusaini mkataba mpya. Pirlo anaamini klabu yeyote itakayomuhitaji Pogba italazimika kulipa zaidi ya euro milioni 100, kiasi ambacho ni sawa na kile Real Madrid waliochoilipa Tottenham Hotspurs kwa ajili ya kumchukua Gareth Bale mwaka 2013. Akihojiwa Pogba amesema anafahamu kuwa Juventus wanataka kubaki na Pogba lakini muda mwingine unaweza kupewa ofa ambayo inaweza kusaidia kutengeneza upya kikosi chao hivyo hadhani kama watakataa.

No comments:

Post a Comment