WAKALA wa Romelu Lukaku, Mino Raiola amedai kuwa mshambuliaji huyo anaweza kuondoka Everton na kuhamia kwa mabingw awa Serie A Juventus majira ya kiangazi. Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji amekuwa na msimu mzuri Merseyside msimu huu, akifunga mabao 18 katika mechi 29 za Ligi Kuu alizocheza. Klabu kadhaa zimeonyesha kuvutiwa kumsajili Lukaku lakini Raiola sasa amefungua milango ya kuweza kwenda Juventus, wakati pia akisisitiza Paris Saint-Germain na Real Madrid nao wanaweza kumuwania. Akihojiwa Raiola amesema Lukaku anaweza kwenda Juventus lakini kuna timu zingine za kuziangalia ambazo pia zimeonyesha nia nazo ni Madrid na PSG.
No comments:
Post a Comment