MENEJA wa Leicester City amesema kikosi chake kinafurahia msimu wa maajabu na wanaweza kuhimili shinikizo katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu. Leicester wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama tisa dhidi ya Tottenham Hotspurs huku kukiwa kumebaki mechi sita kufuatia ushindi wa bao 1-0 waliopata dhidi ya Southampton. Akihojiwa Ranieri raia wa Italia amesema hana shaka kabisa kwani wanafanya kile ambacho wanaamini kinawezekana. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa kila mtu alikuwa akiwaangalia kuona jinsi watakavyofanya baada ya Tottenham kupata sare ya bao 1-1 na Liverpool na wametoa jibu zuri kwa ushindi waliopata. Leicester sasa wanahitaji alama 12 katika mechi sita za mwisho ili kujihakikishia ubingwa wa ligi.
 
 

 
No comments:
Post a Comment