MENEJA wa Manchester United, Louis van Gaal amedai ushindi wa bao 1-0 waliopata katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Everton ni kama wameuiba. United walifanikiwa kupiga mashuti mawili pekee yaliyolenga lango la Everton na bahati moja kati ya hilo liliwasaidia kupata bao kupitia kwa Antony Martial. Akihojiwa Van Gaal amesema hawakucheza vyema kabisa kwani hawakutengeneza nafasi za kutosha. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa Everton ni timu nzuri, imara haswa inapokuwa ugenini hivyo anajiona kama walikuwa na bahati tu katika mchezo huo.

No comments:
Post a Comment