Monday, April 4, 2016

WENGER AMPA TANO CHIPUKIZI WA NIGERIA IWOBI.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger ana uhakika Alex Iwobi ana kitu cha ziada baada ya chipukizi huyo wa kimataifa wa Nigeria kufunga bao lake la pili katika Ligi Kuu kwenye ushindi wa mabao 4-0 waliopata dhidi ya Watford Jumamosi iliyopita. Iwobi ambaye alifunga bao lake la kwanza akiwa na kikosi cha kwanza cha timu hiyo Machi 19 katika mchezo dhidi ya Everton, pia alisaidia kutoa pasi ya mwisho katika bao lililofungwa na Alexis Sanchez. Wenger amesema mashabiki wameshawaona wachezaji wengi wazuri kwa miaka mingi hivyo wanajua mara moja pindi wanapoona mchezaji akiwa na kitu cha ziada. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa ni vigumu kuwadanganya watu kwani wamekuwa wakishuhudia wenyewe jinsi gani Iwobi anavyoimarika haraka na anavyocheza vizuri. Wenger amesema ni mategemeo yake chipukizi huyo ataendelea na jitihada alizonazo ili aweze kuimarika zaidi.

No comments:

Post a Comment