Monday, April 4, 2016

ANCELOTTI ADAI ZIDANE ALIMFANYA ABADILI MBINU ZAKE.

MENEJA wa zamani wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amebainisha kuwa Zinedine Zidane alimbadilisha jinsi alivyokuwa akifikiri kuhusu mchezo wa soka na kumfanya abadilishe mbinu zake za ufundishaji. Meneja huyo raia wa Italia, alichukua mikoba ya kuinoa Juventus mwaka 1999, huku akiwa na nia ya kutumia mfumo wa 4-4-2. Hata hivyo, haraka Ancelotti aligundua kuwa Zidane ana kipaji cha kipekee na namna pekee ya kumfanya awepo katika kikosi chake cha kwanza ni kubali mfumo na kuanza kutumia aina mpya 4-3-1-2. Mfumo wa huo ulishindwa kumsaidia kunyakuwa mataji katika misimu miwili iliyofuata lakini ulikuja kufanikiwa katika klabu yake iliyofuata ya AC Milan ambapo alishinda mataji nane katika kipindi cha miaka nane. Akihojiwa Ancelotti amesema mara ya kwanza alipomuona Zidane ilikuwa ni msimu wake wa kwanza Juventus na nguli ndio alikuwa chanzo cha yeye kubadili mfumo wake aliokuwa akipenda kuutumia.

No comments:

Post a Comment