Monday, April 11, 2016

RANIERI AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUTOBWETEKA.

MENEJA wa Leicester City, Claudio Raniery amesema mashabiki wanaweza kuanza kuota ubingwa lakini wachezaji wake hawapaswi kubweteka baada ya kukaribia kutwaa taji ya Ligi Kuu kwa ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Sunderland. Meneja huyo raia wa Italia alishindwa kuzuia hisia zake wakati alipokuwa akishangilia matokeo ambayo yamewafanya kubakisha ushindi katika mechi tatu ili watawadhwe mabingwa wapya. Akihojiwa Ranieri amesema unapokuwa kocha lazima uwe na hisia haswa timu inapofanya vyema lakini ni vigumu kuelezea ni hisia za aina gani haswa. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa mashabiki lazima waendelee na ndoto zao lakini kwa upande wao wanapaswa kuendelea kuwa makini na kutobweteka kwani kazi bado haijaisha.

No comments:

Post a Comment